Serikali kupiga jeki sekta ya uchumi Samawati na Uvuvi

Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na ununuzi wa mashua za kasi za kupiga doria ununuzi wa vifaa vya kielektroniki vya kufanya uchunguzi na doria baharini.

Dismas Otuke
2 Min Read

Serikali imejitolea kuboresha sekta ya uchumi samawati na uvuvi hapa nchini, ambayo inatoa mchango mahususi kwa pato la kitaifa.

Akizungumza Jumatatu usiku katika Makao Makuu ya afisi ya Msemaji wa Serikali, katibu wa wizara ya Uchumi Samawati na Uvuvi Betsy Muthoni Njagi, alisema mikakati ya kukabiliana uvuvi haramu imewekwa katika ziwa Victoria na Bahari Hindi.

Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na ununuzi wa mashua za kasi za kupiga doria, ununuzi wa vifaa vya kielektroniki vya kufanya uchunguzi na doria baharini.

Aidha bi Njagi alifafanua kuwa serikali imekamilisha ujenzi wa vituo vinane vya kuopoa samaki na tayari imeongeza vingine 15, vikiwemo tisa katika eneo la Nyanza kwa gahrama ya shilingi bilioni 3.6,vilivyozinduliwa na Rais William Ruto mwaka jana.

Kuhusu uchimbaji madini haramu Katibu Njagi, amesema wamebuni vyama vya ushirika kwa wachimbaji madini ili iwe rahisi kuwahamasisha na kuhakikisha serikali za kaunti zinatoa leseni kwa wachimbaji madini halali kupitia vyama vyao vya ushirika.

Bi Njagi alikuwa azingumza kwenye makala ya BongaNaSpokes, yaliyoongozwa na msemaji wa serikali Dkt. Isaac Mwaura Jumatatu usiku.

Mwaura alisema kuwa serikali inatilia mkazo zaidi uchumi samawati na uvuvi wiki hii ambayo itakuwa kauli mbiu kuu ya sherehe za mwaka huu za Madaraka dei Jumapili hii katika kaunti ya Homa Bay.

Share This Article