Sunderland imewalemea Sheffield United mabao 2-1 kwenye fainali ya kupandishwa ngazi hadi EPL iliyochezwa Jumamosi jioni katika uwanja wa Wembley, wakirejea ligini baada ya subira ya miaka minane na ushindi wa kwanza wa mechi hiyo ya mchujo baada ya kushindwa mara tano.
Sheffield United, waliomaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Championship walichukua uongozi kunako dakika ya 25 kupitia kwa Tyrese Campbell,kabla ya Patrick Roberts kusawazisha dakika 15, kabla ya kipenga cha mwisho.
Tom Watson alipachika kimiani bao la ushindi katika sekunde za mwisho na kuwanyanyua mashabiki kwa sherehe za kina aina .
Sunderland maarufu kama Black Cats wamerejea ligini kwa mara ya kwanza tangu walipushwa daraja msimu wa mwaka 2016/2017.