Uchaguzi wa NOCK kuandaliwa Juni 19

Uchaguzi huo uliaharishwa Aprili 13, baada ya mashirikisho manne ya michezo kukosa kuelewana kuhusu wapiga kura wao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uchaguzi wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki nchini Kenya – NOCK, ambao umesubiriwa kwa hamu na ghamu, sasa utaandaliwa tarehe 19 mwezi ujao.

Jumla ya viti 13 vinawaniwa katika uchaguzi huo vikiwemo Rais, Naibu Rais wa kwanza, Naibu Rais wa pili, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina na Naibu wake, wanachama watatu wa kamati kuu, mwakailishi wa wanawake, na waakilishi wawili wa wananamichezo (mmoja wa kiume na mwanamke mmoja).

Uchaguzi huo uliaharishwa Aprili 13, baada ya mashirikisho manne ya michezo kukosa kuelewana kuhusu wapiga kura wao.

Watakaochaguliwa watahudumu kwa kipindi cha miaka minne afisini.

Share This Article