Ukraine na Urusi zabadilishana mamia ya wafungwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Russia na Ukraine zabadilishana wafungwa. Picha/Hisani.

Katika kile kinachoonekana kama hatua za kusitisha vita kati ya Ukraine na Russia, nchi hizo mbili zimebadilishana mamia ya wafungwa, hii ikiwa idadi kubwa zaidi tangu kuanza kwa vita mwaka 2022.

Katika mabadilishano hayo, nchi hizo mbili zimerejesha wanajeshi 270 na raia 120 kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus, kama sehemu ya makubaliano yaliyokubaliwa katika mazungumzo ya moja kwa moja huko Istanbul wiki moja iliyopita.

Pande zote mbili zilikubaliana kubadilishana wafungwa 1,000 na kuthibitisha kutakuwa na mabadilishano zaidi katika siku zijazo.

Urusi na Ukraine ziliandaa mkutano wa ana kwa ana,kujadili mchakato wa kumaliza vita baina yao, ambavyo vimesababisha vifo, majeraha na wengi kupoteza makao.

TAGGED:
Share This Article