KCB yapiga teke dawati la ukufunzi kwa matokeo duni

Mkufunzi wa walinda Samuel Koko Okoth, ameteuliwa kaimu kocha kwa mechi mbili za kuhitimisha msimu huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Kenya Commercial Bank-KCB, imewasimamisha kazi kwa muda maafisa wote wa dawati la ukufunzi kutokana na matokeo mabovu.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, KCB imewapiga marufuku mara moja kocha mkuu Patrick Odhiambo, msaidizi wake Jeffer Odongo, na manyanyishaji mazoezi Eric Muranda.

Mkufunzi wa walinda Samuel Koko Okoth, ameteuliwa kaimu kocha kwa mechi mbili za kuhitimisha msimu huu.

“Tumefanya mazungumzo ya pamoja na kocha na wasidizi wake wawili . Tunataka kuongeza ari na nguvu kwa timu ili imalize msimu vyema na kujiandaa vyema kwa msimu ujao.” amesema Mwenyekiti wa KCB Bramwel Simiyu

Wahifadhi hela KCB wanakalia nafasi ya tisa ligi kwa alama 41, kutokana na mechi 32 wakishinda 10, kutoka sare 11 na kupoteza 11.

KCB watawaalika Nairobi City Stars Juni 10 kabla ya kufunga msimu ugenini dhidi ya AFC Leopards siku tano baadaye.

Share This Article