Ni kivumbi Italia leo, Inter Milan,Napoli wakipigania ubingwa wa Serie A

Inter Milan watakuwa na kibarua ugenini watakapomenyana na Como inayonolewa na Cesc Fabregas wakati Napoli wakiwa nyumbani dhidi ya Cagliari.

Dismas Otuke
1 Min Read
epa12115243 Napoli's coach Antonio Conte (L) and his player greet their supporters after the Italian Serie A soccer match between Parma Calcio and SSC Napoli, in Parma, Italy, 18 May 2025. EPA/ELISABETTA BARACCHI

Kivumbi kinatarajiwa leo usiku kuanzia saa tatu na dakika 45 majira ya Kenya, wakati wa kuchezwa kwa mechi mbili za Ligi Kuu Italia, Serie A, kubaini mabingwa wa Ligi msimu wa mwaka 2024/2025.

Inter Milan watakuwa na kibarua ugenini watakapomenyana na Como inayonolewa na Cesc Fabregas wakati Napoli wakiwa nyumbani dhidi ya Cagliari.

Napoli wanahitaji ushindi wowote ili kutawazwa mabingwa, ingawa pia watatwaa kombe kwa kutokuwa na sare endapo wapinzani wao Inter watapoteza au pia kuambulia sare.

Inter ni sharti washinde na kutarajia Cagliari watawashinda Napoli ili kunyakua scudetto.

Napoli wanaongoza jedwali kwa pointi 79 baada ya mechi 37, pointi moja juu ya Inter Milan.

Share This Article