Serikali ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati kwa gharama ya shilingi bilioni 700 za Tanzania, sawia na shilingi bilioni 34 za Kenya.
Daraja hilo la umbali wa kilomita 3 kupitia ziwani Victoria lililopewa jina la JP Magufuli, na linaunganishwa na barabara ya umbali wa kilomita 1.6, kutoka Kigongo hadi Busisi .
Daraja hilo lilipewa jina kwa heshima ya Hayati Rais Magufuli, na linatarajiwa kufungua biashara katika ukanda wa maziwa makuu.