Serikali yatoa shilingi bilioni 22 kufadhili masomo

Kwa mujibu wa waziri wa Elimu Julius Ogamba, fedha hizo ni asilimia 30 ya pesa zote za serikali kuu kugharamia masomo kwa shule za umma mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read
Julius Ogamba, Waziri wa Elimu

Serikali imetoa shilingi bilioni 22.03, za kufadhili masomo katika shule za msingi na za upili za umma kwa mhula wa pili .

Pea hizo ambazo zimetolewa  majuma matatu tangu kufunguliwa kwa muhula wa pili katika mwaka wa masomo wa 2025.

Kwa mujibu wa waziri wa Elimu Julius Ogamba, fedha hizo ni asilimia 30 ya pesa zote za serikali kuu kugharamia masomo kwa shule za umma mwaka huu.

Kati ya kiwango hicho, shilingi bilioni 1.37 zitagharamia masomo ya bure kwa shule za msingi, bilioni 8.9 zielekezwe kugharamia masomo ya bure kwa shule za Junior Secondary, milioni 118 kwa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum na bilioni 11.6 kwa shule za sekondari za umma za kutwa.

Share This Article