Rais Ruto kukabidhi zaidi ya nyumba 1,000, kesho mtaani Mukuru

Vyumba hivyo vya gharama nafuu vimejengwa katika kipande cha ardhi cha ekari 56 kikiwa na jumla ya vyumba 13, 248 .

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Ruto kesho, Jumanne, anatarajiwa kukabidhi zaidi ya nyumba 1,000, kwa wakazi wa mtaani Mukuru, katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za kaunti ndogo ya Embakasi Kusini.

Vyumba hivyo vya gharama nafuu vimejengwa katika kipande cha ardhi cha ekari 56 kikiwa na jumla ya vyumba 13, 248 .

Mradi huo ndio mkubwa zaidi nchini katika mpango wa mfumo wa uchumi wa Bottom Up, ambao unalenga kujenga nyumba mpya laki mbili kila mwaka.

Share This Article