Makala ya sita ya mbio za Kip Keino Classic Continental Tour, yataandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, baada ya kuhamishwa kutoka uwanja wa taifa wa Nyayo tarehe 31 mwezi huu.
Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir, amesema wamelazimika kuhamishia mashindano hayo Ulinzi kutokana na kucheleweshwa ukitaji wa zulia katika uwanja wa Nyayo.
Hata hivyo, Korir amesisitiza kuwa kamwe kubadilishwa kwa uwanja hakutaathiri hadhi ya mashindano ila tu idadi ya mashabiki watakaoingia uwanjani.
Itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo kuandaliwa nje ya viwanja vya desturi vya Nyayo na Kasarani tangu yajumuishwe kwenye kalenda ya shirikisho la Riadha Ulimwenguni mwaka 2020.