Mipango ya mazishi ya Nkechi Nweje yatangazwa

Marion Bosire
0 Min Read

Familia ya marehemu mwigizaji wa filamu nchini Nigeria Bi. Nkechi Nweje imetangaza mipango ya mazishi yake.

Katika bango lililochapishwa na mwigizaji mwenza Rita Edochie imebainishwa kwamba mwendazake atazikwa Ijumaa Mei 23, 2025 huko Onitsha katika Jimbo la Anambra nchini Nigeria.

Rita alifafanua kwamba alipata bango hilo kutoka kwa familia ya Nkechi ambaye anamrejelea kama mkwe wake.

Nkechi alifariki Machi 21, 2025 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Share This Article