Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, atafanya ziara ya kiserikali nchini Marekani juma lijalo, imesema taarifa kutoka afisi ya Rais wa Afrika Kusini.
Ziara hiyo ya Washington DC ianatarajiwa kuanza Mei 19 hadi 21, 2025, ambapo Rais Ramaphosa na mwenyeji wake Donald Trump watajadili maswala kati ya nchi hizo mbili, za kanda na ulimwengu kwa jumla.
Siku ya Jumatano,Mei 21, 2025, Rais Ramaphosa atakutana na Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House Jijini Washington DC kujadili masuala yanayohusu nchi hizo mbili, kikana na kimataifa,” ilisema taarifa ya Afisi ya Rais wa Afrika Kusini kupitia ukurasa wa X.
Kulingana na taarifa hiyo, ziara hiyo inatoa fursa ya kujenga upya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Uhusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani umedorora sana tangu Trump arejee Ikulu ya Marekani mnamo mwezi Januari mwaka 2025.
Wiki hii utawala wa Trump ulikaribisha wazungu 49 wa Afrika Kusini ambao umewapa hadhi ya ukimbizi, baada ya kuwachukulia kuwa wahanga wa ubaguzi wa rangi.