Simba yasaka historia nchini Morocco

Tayari tiketi zote za kuingia uwanjani kwa Mkappa Mei 25, kwa mechi ya marudio kati ya Simba na Berkane zimeuzwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka Tanzania bara klabu ya Simba watalenga kuandikisha historia kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kutwaa kombe la shirikisho, watakapomenyana na wenyeji RS Berkane ya Morocco, katika mkumbo wa kwanza wa fainali kuwania kombe la Shirikisho.

Simba walipiga mazoezi ya kwanza jana jijini Casablanca, punde baada ya kuwasili kwa nchini humo.

Wekundu wa Msimbazi  watachuana na Berkane  Jumamosi hii,Mei 17, kuanzia saa nne usiku, kabla ya kuandaa mechi ya marudio katika uwanja wa Benjamin Mkappa tarehe 25.

Tayari tiketi zote za kuingia uwanjani kwa Mkappa Mei 25, kwa mechi ya marudio kati ya Simba na Berkane zimeuzwa.

Share This Article