Shirika la Maendeleo ya Wanawake, limezindua usajili wa waanachama katika wadi zote 1,450 zilizopo katika kaunti zote 47, ili kujiandaa kwa uchaguzi wa kitaifa ulioratibiwa kuandaliwa mwaka 2028.
Mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi Anne Wambaa, alisema kuwa shughuli ya usajili wanachama ilianza Mei 14 na itaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo, Wambaa alisisitiza kuwa ni wanachama ambao wamesajiliwa; wataruhusiwa kupiga kura na kuwania nyadhfa katika uchaguzi ujao.
Upande wake Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo, Isabela Ndolo, alisema usajili wa wanachama utakamilika Januari mwaka ujao, kabla ya kupisha uchaguzi wa mashinani.
Wanachama wanapaswa kulipa ada ya shilingi 1,000, ili kusajiliwa na kupata fursa ya kushiriki katika uchaguzi.
Hata hivyo, yeyote anayenuia kuwania wadhfa wa uongozi chamani ni sharti awe mwanachama kwa muda usiopungua miaka 10.