Bei ya bidhaa za Petroli yakosa kubadilika kwa Mwezi wa tatu mfululizo

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya kudhibiti bei za bidhaa za Petroli hapa nchini EPRA, imetangaza kutobadilika kwa bei za mafuta kwa mwezi watatu mfululizo.

Katika tangazo lake, EPRA imesema imetumia hazina ya kudhibiti bei kuhakikisha bei ya bidhaa za Petroli haiongezeki.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa kuanzia usiku wa kuamkia Alhamisi, Jijini Nairobi bei ya Petroli itasalia kuuzwa shilingi 174.63, Ile ya Diesel Shilingi 164.86 na mafuta taa shilingi 148.99.

“EPRA ingependa kuhakikisha umma kwamba imejitolea kulinda maslahi ya wateja na wawekezani katika sekta ya nishati na mafuta,” alisema Mkurigenzi Mkuu wa EPRA Daniel Kiptoo,

TAGGED:
Share This Article