Maeneo nchini yanatarajiwa kuendelea kupokea mvua kubwa katika kipindi cha wiki moja ijayo.
Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa, maeneo ya nyanda za kati, Nairobi, maeneo ya Ziwa Victoria, bonde la ufa na magharibi mwa nchi yataendelea kupokea viwango vya juu vya mvua.
Hali kadhalika sehemu nyingi nchini zitasalia kuwa na unyevunyevu.