Kenya yanyakua shaba mita 400 mbio za Dunia kupokezana kijiti

David Kapirante alikuwa mwenye kasi zaidi akikamilisha mzunguko wa kwanza kwa sekunde 45.98

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti mseto imenyakua nishani ya shaba katika mashindano ya Dunia yanayoendelea mjini Guangzhou, China.

David Kapirante alikuwa mwenye kasi zaidi akikamilisha mzunguko wa kwanza kwa sekunde 45.98, naye Mrcy Chebet, akamaliza mzunguko wa pili kwa kutumia sekunde 49.77, huku Brian Tinega, akipiga mzunguko wa tatu kwa dakika kwa sekunde 45.93 .

Mercy Oketch amekamilisha mzunguko wa mwisho kwa sekunde 51.42, huku timu hiyo ikimaliza ya tatu kwa muda wa dakika 3 sekunde 13.10 .

Marekani imenyakua dhahabu kwa kuweka rekodi moya ya mashindano ya dakika 3 sekunde 9.54, huku Australia ikiridhia fedha.

 

Share This Article