Mwanamuziki wa Tanzania Harmonize amesema kwamba mwanamuziki mwenza Ibraah ambaye ni msajiliwa wa kampuni yake ya muziki ya Konde Music Worldwide ni mtu mwenye wivu.
Matamshi yake yanatokana na tangazo alilota Ibraah kwamba Harmonize anamdai shilingi Bilioni moja kabla ya kumruhusu kuondoka kwenye kampuni hiyo.
Kupitia Insta Stories leo, harmonize amesema kwamba baada ya kuchunguza, ameona kwamba Inbraah ambaye pia hujiita Chinga ni mtu mwenye wivu na inaonekana ibilisi amempanda kichwani.
Kulingana na Konde Boy, Chinga aliona kwamba yeye anazungumziwa sana mitandaoni kwa mazuri akaona kwamba amchafulie sifa.
Anasema Ibraah alichagua siku ambayo walikuwa wanasherehekea siku ya kuzaliwa ya mjukuu wa Kajala ambapo ilidhihirika kwamba wamerudiana na Kajala na hivyo kuzungumziwa sana mitandaoni, kuwa siku ya kuchapisha madai kwamba amemtaka amlipe pesa hizo.
Harmonize amefafanua kwamba hajamwomba Chinga Bilioni moja ila ni mahitaji ya mkataba ambao alitia saini na kampuni ya Konde Music na kwamba kampuni hiyo iliwekeza pesa nyingi kwake ambazo Harmonize anasema alikopa.
Sasa anahimiza umma umchangie ili atimize Bilioni moja baada yake mwenyewe kudaiwa kumchangia shilingi laki moja pesa za Tanzania.
Lakini Ibraah tena alijikanganya juzi alipotangaza kwamba ametumia sehemu ya pesa alizochangiwa kugharamia matibabu ya mamake mzazi isijulikane lengo kamili la mchango anaoendesha ni lipi.