Bunge la Ulaya –EU, limeshinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema, Tundu Lissu, kuachiliwa kutoka korokoroni na serikali mara moja bila vikwazo.
Bunge hilo lililojadili hoja hiyo Mei 7, lilisikitishwa na matukio ya kisiasa nchini Tanzania, kuelekea kwa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha, limeitaka serikali kuondoa makossa ya uhaini aliyoshtakiwa nayo Lissu.