Baraza la Mawaziri la Israel, laidhinsha kutwaliwa kwa Gaza yote

Pia taarifa imetolewa kwa mamia ya maelfu ya watu walio Gaza kuhamia kusini mwa eneo hilo.

Dismas Otuke
1 Min Read
Benjamin Netanyahu - Waziri Mkuu wa Israel

Hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi eneo la Gaza nchini Palestina, kufuatia hatua ya Baraza la Mawaziri la Israel siku ya Jumatatu kuidhinisha kutwaliwa kwa ukanda huo wote kwa muda usiojulikana.

Pia taarifa imetolewa kwa mamia ya maelfu ya watu walio Gaza kuhamia kusini mwa eneo hilo.

Msemaji wa jeshi la Israel Brigedia Effie Defrin, amesema lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha mateka wote wa Israel, wamerejeshwa na kuangamiza kundi la Hamas.

Haya yanajiri wakati ambapo Mkuu wa Majeshi ya Israel, alipotangaza kuwaita zaidi ya wanajeshi 10,000, wa kiba kujiunga na oparesheni hiyo.

Share This Article