Botswana yajiondoa kutetea taji ya mbio za kupokezana kijiti duniani

Makala ya mwaka huu ya mbio za kupokezana kijiti duniani yataandaliwa mjini Guanzhou, Uchina, kati ya Mei 10 na 11.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Botswana, imejiondoa kutetea taji ya dunia ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume mwaka huu.

Wanariadha watatu wakiongozwa na bingwa wa Olimpiki katika mita 200, Letsile Tebogo, Collen Kebinatshipi, na Bayapo Ndori, wamejiondoa kutokana na sababu za kibinafsi.

Timu hiyo ilishinda dhahabu katika mbio za kupokezana kijiti duniani mwaka jana mjini Nassau, Bahamas, kabla ya kunyakua nishani ya fedha katika michezo ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.

Makala ya mwaka huu ya mbio za kupokezana kijiti duniani yataandaliwa mjini Guanzhou, Uchina, kati ya Mei 10 na 11.

Share This Article