Wakili Peter Kibatala ambaye ni mmoja wa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema mwanasiasa huyo amepanga kususia kula chakula gerezani Ukonga,kushinikiza haki itendeke katika mashitaka ya uchochezi na uhaini yanayomkabili katika Mahakama ya Kisutu.
Akiongea siku ya Jumamosi Jijini Dare salaam, Kibatala amesema “Natoa taarifa rasmi kwa Umma kwa niaba ya Mteja wetu kwamba anaanza kususia chakula, sio kwasababu nyingine bali anataka haki itendeke, tutatoa taarifa rasmi kuhusu siku hasa lakini atasusa kula chakula kitakachomtokea yupo tayari, hatokula chakula mpaka pale atakapoona haki inatendeka”
“Lissu ni Wakili Mkongwe , Sisi wengine mojawapo ya Majabali yaliyotufanya tusome sheria namna hii tunayofanya ni huyu Mtu, haogopi kesi, hata kama sisi tusingekuwepo angeendesha kesi mwenyewe, haogopi kesi anataka haki itendeke, atasusia kula chakula mpaka haki itakapotendeka”
Katika hatua nyingine Lissu kupitia ukurasa wake wa X, ametoa taarifa kuwa endapo hatopelekwa Mahakamani Maei 6,2025 ataanza rasmi kugoma kula chakula.