Patachimbika Gusii Stadium ,Shabana ikiwaalika Gor Mahia, kesho

Gor wanakalia nafasi ya tatu kwa pointi  50, alama 4 mbele ya Shabana iliyo ya nne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kivumbi kinataraijiwa kesho adhuhuri katika uwanja wa Gusii ,wakati wenyeji Shabana FC watamenyana na mabingwa watetezi Gor Mahia FC katika mchuano wa ligi kuu.

Timu zote zilitoka sare katika duru ya kwanza Novemba mwaka  jana.

Gor wanakalia nafasi ya tatu kwa pointi  50, alama 4 mbele ya Shabana iliyo ya nne.

Shabana wanajivunia  kusvheza mechi 11 nyumbani bila kushindwa huku K’ogalo wakienda mechi tisa bila ksuhindwa uegnini.

Tiketi za mechi hiyo zinauzwa kwa shilingi 300, kwa zile za maeneo ya kawaida ,shilingi 1,000 kwa zile za VIP na shilingi 3,000 kwa zile za VVIP.

Mchuano huo maarufu kama Nyanza Derby, unatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi.

Share This Article