Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA,imeamrisha kushushwa ngazi kwa kilabu ya Muhoroni Youth kutoka ligi ya daraja ya kwanza -NSL, hadi ile ya FKF Divisheni ya kwanza, baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki upangaji matokeoya mechi nchini.
FIFA tayari imewasiliana na shirikisho la FKF, ili kuhakisha utekelezaji kikamilifu kwa amri hiyo.
Muhoroni ilishushwa ngazi kutoka Ligi Kuu FKF mwishoni mwa msimu jana baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 kati ya timu 18 zilizohiriki ligi.
Uchunguzi wa kesi ya upangaji matokeo ya mechi dhidi ya Muhoroni Youth, umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo bado walikuwa wanakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja kutoka NSL hadi divisheni ya kwanza msimu ujao wakikalia nafasi ya 18 kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu.