Rais William Ruto, amemteua Prof. Makau Mutua kuwa Mshauri Mkuu wa maswala ya katiba katika afisi ya Rais.
Kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumatano, kiongozi wa taifa alisema Prof. Mutua analeta tajiriba ya kisheria, kikatiba na maswala ya haki za binadamu.
“Hongera Prof Mutua. Nakukaribisha kujiunga na kundi la watumishi wa umma katika kutekeleza ajenda yetu ya kuimarisha uchumi kuanzia chini,” alisema Rais Ruto.
Huku akikubali uteuzi huo, Profesa huyo wa sheria aliahidi kuitumikia serikali na wananchi kwa heshima na kwa njia ya kipekee.
“Ninamshukuru Rais William Ruto kwa kuniteua kuwa Mshauri Mkuu wa maswala ya katiba katika afisi ya Rais,” alisema Prof. Mutua.