Washirika wa kimataifa waungana na Kenya kufanikisha usalama Kaskazini Mashariki

Tom Mathinji
2 Min Read

Balozi tano zimeshirikiana na serikali ya taifa na zile za kaunti katika eneo la Kaskazini Mashariki, kushughulikia ukosefu wa usalama na changamoto za kimaendeleo.

Uingereza, Marekani, Muungano wa ulaya, Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa zimeshirikiana kuchochea maendeleo na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

Kulingana na washirika hao, eneo la Kaskazini Mashariki ni muhimu sana taifa hili, kwa kuwa lina utajiri wa rasilimali na uwezo wake mkubwa wa kuleta udhabiti katika Kanda hiyo.

Miongoni mwa maswala ambayo yanapewa kipaumbele ni pamoja na kudumisha amani na usalama, kukabiliana na itikadi kali, mizozo ya kijamii na kukuza Imani katika taasisi za umma.

Mengine ni kukabiliana na Tabia Nchi na kiangazi, usawa wa kijinsia katika uongozi, elimu na fursa za kiuchumi nà kuimarisha utoaji wa huduma.

Mshirikishi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Stephen Jackson, alisema wanajizatiti kuleta maendeleo na usalama katika eneo hilo

“Eneo hili lina uwezo mkubwa kuanzia mifugo, kilimo, nishati mbadala na uchimbaji madini,” alisema mshirikishi huyo.

“Kati ya mwaka  2017 na mwaka huu, tumewekeza jumla ya shilingi bilioni 188 katika eneo hili,” aliongeza Jackson .

Eneo la Kaskazini Mashariki kwa muda mrefu limekilnwa visa vya ukosefu wa usalama na changamoto za maendeleo zinazosabanishwa na mashambulizi ya Al Shabab.

Mrakibu wa eneo la Kaskazini Mashariki John Otieno alisema serikali imeweka mikakati ya kudumisha usalama Kupitia operesheni za kukabiliana na wahalifu.

“Tunazingatia kuwawezesha vijana na wanawake ili washiriki kikamilifu kwa shughuli za maendeleo,” alidokeza Otieno.

 

Share This Article