Watu 15 wafariki kwenye mkasa wa moto India

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 15 wafariki kwenye mkasa wa moto katika hoteli moja nchini India.

Watu 15 wamefariki kwenye mkasa wa moto uliotokea katika hoteli moja mjini Kolkata, nchini India.

Kulingana na maafisa wa polisi nchini humo, watu kadhaa pia walijeruhiwa kwenye mkasa huo walipokuwa wakitoroka kupitia madirishani na wengine kutumia paa.

“Watu kadhaa waliokolewa kupitia paa za hoteli hiyo,” alisema Afisa Mkuu wa polisi wa eneo la Kokata Manoj Verma.

Visa vya kuzuka kwa moto ni maarufu sana nchini India, kutokana na ukosefu wa vifaa vya kukabiliana na moto na hali ya kupuuza masharti ya kiusalama.

Shirika moja la habari nchini humo lilisema kuwa, watu walionekana wakitoroka jengo hilo kupitia madirisha na paa za hoteli hiyo, moto huo ulipozuka.

Afisa huyo mkuu wa polisi hata hivyo alithibitisha kuwa moto huo umezimwa kikamilifu.

TAGGED:
Share This Article