Simba anguruma hadi fainali ya Kombe la Shirrikisho

Timu hizo zimetoka sare kappa katika marudio ya nusu fainali leo jioni baada ya Simba kushinda duru ya kwanza bao moja kwa nunge wiki jana.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka Tanzania bara Simba SC wamefuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kusajili ushindi wa jumla wa bao moja kwa bila dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini katika nusu fainali.

Timu hizo zimetoka sare kappa katika marudio ya nusu fainali leo jioni baada ya Simba, kushinda duru ya kwanza bao moja kwa nunge wiki jana.

Simba watapambana na RS Berkane ya Morocco kwenye fainali .

Mashabiki wa Simba walifurika mitaani Dares Salaam kufuatilia mechi ya Jumapili jioni kupitia kwa runinga, wengi wakivalia sare za wekundu wa Msimbazi.

 

 

Share This Article