Atwoli aitaka serikali kudhibiti mitandao ya kijamii

Atwoli aitaka serikali kudhibiti mitandao ya kijamii

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu Mkuu wa chama cha wafanyikazi nchini COTU, Francis Atwoli, ameitaka serikali kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii humu nchini.

Akiwahutubia wanahabari leo, Atwoli, amesema vijana wengi wanatumia vibaya mitandao kwa kuchapisha habari ambazo hazifai kwa watu wenye umri mdogo na kuifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yaliyo na mitandao inayohatarisha maisha ya wengi.

Akitoa mfano wa China, ambapo serikali hudhibiti mitandao ya kijamii, Atwoli amelitaka kanisa na serikali kuzungumzia haswa matumizi mabaya ya mtandao wa TikTok.

Matamshi ya Atwoli yanajiri wakati ambapo baadhi ya viongozi wanashinikiza kudhibitiwa kwa matumizi ya mitandao ili kuzuia matumizi mabaya.

Share This Article