Ndoto ya vipusa wa Kenya kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili yazimwa

Kenya waliokuwa wamelazwa goli moja kwa bila katika duru ya kwanza walishindwa kwa jumla ya mabao 4-1 na Cameroon.

Dismas Otuke
1 Min Read

Matumaini ya timu ya taifa ya Kenya kwa wanawake chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets, kushiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia yalizimwa jana usiku, baada ya kushindwa na wenyeji Cameroon mabao 3-1 katika maraudio ya raundi ya tatu.

Kenya waliokuwa wamelazwa goli moja kwa bila katika duru ya kwanza walishindwa kwa jumla ya mabao 4-1 na Cameroon.

Cameroon imefuzu kushiriki makala ya 9 ya kipute cha Kombe la Dunia kitakachoandaliwa nchini Morocco, kati ya Oktoba 17 na Novemba 8 mwaka huu.

Share This Article