Mkenya Agnes Jebet Ngetich, ameandikisha rekodi mpya ya dunia ya mbio za kilomita 10 kwa wanawake pekee.
Bingwa huyo wa Sirikwa Classic mwaka huu alisajili muda wa dakika 29 na sekunde 27 katika mashindano ya Adizero Road to Records mjini Herzogenaurach, nchini Ujerumani, mapema Jumamosi.
Jebet amevunja rekodi ya marehemu Agnes Jebet, ya mwaka 2021 ya dakika 29 na sekunde 30, akiwa mwanamke wa kwanza kuzikamilisha mbio hizo chini ya muda wa dakika 29 na sekunde 30.
Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 24 pia anashikilia rekodi ya kilomita 10 kwa wanaume na wanawake you dakiak 28 na sekunde 46.