Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesmema kuwa mizozo ya ardha ni miongoni mwa maswala ambayo yamechangia pakubwa kwa ukosefu wa usalama kaunti ya Machakos.
Murkomen aliyasema hayo leo Jumamosi, aliposhiriki mkutano na kamati ya usalama ya kauti ya Machakos, ambapo walijadili changamoto za kiusalama na suluhu za kukabiliana na changamoto hizo.
“Maswala muhmu yaliibuliwa kama vile unyakuzi wa ardhi unaotekelezwa na magenge ya wahalifu, pombe haramu, uharibifu wa miundomsingi muhimu na mizozo kati ya binadamu na wanyamapori,” alisema Murkomen kupitia ukurasa wake wa X.
Waziri huyo alisema wizara yake itaandaa ripoti itakayotumika kubuni sera ya kitaifa kushughulikia mizozo ya umiliki ardhi hususan katika kesi zinazohusisha umili wa mashamba makubwa ambayo yamevamiwa na maswota na wanyakuzi wa ardhi.
Murkomen yuko katika kaunti ya Machakos ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika eneo la Mashariki mwa nchi, kukadiria hali ya usalama almaarufu Jukwaa la Usalama.
Waziri huyo alikuwa ameandamana na katibu katika wizara hiyo Dkt. Raymond Omollo, Kamishna wa eneo la Mashariki Paul Rotich, Kamishna wa kaunti ya Machakos Josephine Ouko na maafisa wengine wa ngazi za juu katika wizara hiyo.