Rais Will Ruto amewasili Jijini Rome nchini Italia kuhudhuria mazishi ya Papa Mtakatifu Francis, yanayoandaliwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Kiongozi wa taifa atajiunga na viongozi wengine wa ulimwengu kumuaga kiongozi huyo wa kanisa Katoliki, ambaye anazikwa leo Jumamosi.
“Nimewasili Jiji Rome, Italia, kujiunga na viongozi wengine wa dunia na waumini wa kanisa katoliki kuhudhuria mazishi ya Papa Mtakatifu Francis,” alisema Rais Ruto kupitia ukurase wake wa X.
Viongozi mashuhuri waliothibitisha kuhudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Uhispania, Rais Lula da Silva wa Brazil, na Sultan William kwa niaba ya Mfalme Charles III.
Wengine ni Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Rais wa Poland Andrzej Duda, Rais wa Argentina Javier Milei, Rais wa Italia Sergio Mattarella, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Papa Francis alifarikizJumatatu, Aprili 21, 2025 akiwa na umri wa miaka 88.