Rais Ruto akamilisha ziara ya siku nne nchini China

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto azuru jimbo la kusini mashariki mwa China la Fujian.

Rais William Ruto amekamilisha ziara yake ya kiserikali ya siku nne nchini China kwa kuzuru taasisi za utafiti na kitamaduni kwenye jimbo la kusini mashariki mwa China la Fujian.

Kiongozi wa taifa alianza ziara yake Makao Makuu ya kampuni ya teknlojia ya Contemporary Amperex Technology  Limited (CATL) mjini Ningde.

Kupitia ziara hiyo, Rais Ruto aliipongeza kampuni hiyo ya kimataifa ambayo hutengeneza betri za magari ya umeme, akisema imechangia pakubwa katika utoaji wa kawi safi kwa kuleta mabadiliko katika sekta ya uchukuzi na kuzuia utoaji wa hewa ya Cabon kutoka viwandani.

Rais baadaye alizuru ukumbi wa maonyesho ya mbinu za kukabiliana na umasikini wa Ningde.Alipongeza maono ya viongozi wa sasa na wa zamani wa Ningde akiwemo Rais Xi Jinping, kwa kuondoa mji huo kwenye umasikini.

Baadaye rais Ruto alizuru kituo cha utafiti wa ujenzi cha Fujian Academy, ambacho ni taaasis ya ubunifu wa kisayansi ambayo imejenga miradi mikubwa nchini Kenya ikiwemo barabara ya Turbi-Moyale huko Marsabit na jingo la hazina ya malipo ya uzeeni ya benki kuu ya Kenya.

Rais alikamilisha ziara yake kwa kuzurumaeneo kadhaa ya kihistoria huko Fulhou ambayo huhifadhi na kuonyesha turathi za utamaduni wa nchi hiyo.

Share This Article