Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe,leo ameshauriana na Balozi wa Ufaransa nchini Arnaud Suquet, aliyemtembelea katika makao makuu ya wizara, Kilimo House .
Mazungumzo baina yao yalihusu jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na Ufaransa kwa lengo la kuwa na kilimo endelevu na utoshelezi wa chakula kwa kutumia utaalam wa Ufaransa katika sekta ya kilimo.
Mengine yaliyojadiliwa ni mwafaka wa makubaliano ya mwaka 2023, kuhusu uongezaji tija katika ufugaji wa mifugo na ufufuzi wa ushirikiano kati ya Kenya na Ufaransa kupitia taasisi za kilimo za Ufaransa.