Osaka yapiga marufuku wakongwe kutumia rununu kwenye ATM

Imesemekana kuwa matapeli huwapigia wazee hao simu wakiwa kwenye ATM wakijifanya kuwa watu wa familia, na baadaye kuwashurutisha kuhamisha pesa au kutoa pesa taslimu na kuwaibia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wasimamizi wa mji wa Osaka nchini Japan, wamepigwa marufuku matumizi ya simu za rununu kwa wakongwe zaidi ya umri wa miaka 65 wanapotumia mashine za ATM katika benki.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na ongezeko la walaghai wanaowalenga wazee hao huku takwimu zikiashiria kuwa magenge yalipora dola nusu milioni mwaka jana kutoka kwa kundi hilo la watumiaji mashine za ATM.

Imesemekana kuwa matapeli huwapigia wazee hao simu wakiwa kwenye ATM wakijifanya kuwa watu wa familia, na baadaye kuwashurutisha kuhamisha pesa au kutoa pesa taslimu na kuwaibia.

Sheria hiyo itaanza kutekelezwa Agosti mwaka huu, ingawa hakuna adhabu kwa wakongwe watakaokiuka .

TAGGED:
Share This Article