Timu ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17,ilifanya mazoezi ya kwanza jana mjini Yaoundé, Cameroon, kujiandaa kwa mechi ya marudio raundi ya tatu, kufuzu kwa fainali za Kombe la dunia dhidi ya wenyeji leo jioni.
Kenya ilishindwa bao moja kwa nunge katika duru ya kwanza uwanjani Nyayo Jumapili iliyopita .
Junior Starlets wanawania kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mtawalia baada ya kushiriki mwaka jana kwa mara ya kwanza katika JamhurI ya DominiCa.
Fainali za Kombe la Dunia zitaandaliwa mwishoni mwa mwaka huu nchini Morocco.