Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 20 – Rising Stars, ilitoka sare ya 2-2 na Ghana, katika mchuano wa kujipiga msasa ulioandaliwa jana jioni nchini Misri.
Magoli ya Kenya inayonolewa na kocha Salim Babu ,yalifungwa na Lawrence Ouma na Hassan Beja.
Timu zote zilitumia pambano hilo kujiandaa kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), yatakayoanza kutimua vumbi Jumapili hii nchini Misri.
Kenya itafungua mechi zake kundini B dhidi ya Morocco Mei 1, kabla ya kukabiliana na Tunisia siku tatu baadaye ,na kukamilisha mechi za kundi hilo dhidi ya mabingwa mara saba Nigeria Mei 7.
Rising Stars wanashiriki kipute hicho kwa mara ya kwanza .