Gor Mahia wakatiziwa mawasiliano na Talanta FC

Goli pekee na la ushindi kwa Talanta lilitiwa kimiani na Emmanuel Osoro kunako dakika ya 39.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini, Gor Mahia, wamepigwa na butwaa baada ya kulazwa bao moja bila jibu leo na Talanta FC katika mchuano wa pekee wa Ligi Kuu FKF, uliosakatwa leo uwanjani Dandora, kaunti ya Nairobi.

Goli pekee na la ushindi kwa Talanta lilitiwa kimiani na Emmanuel Osoro kunako dakika ya 39.

Ushindi huo umefufua matumaini ya Talanta kusalia ligi msimu ujao wakizoa jumla ya alama 29 katika nafasi ya 14.

Hata hivyo, Gor Mahia wametia doa juhudi za kuhifadhi ubingwa kufuatia kipigo hicho wakisalia na nambari tatu kwa pointi 47, alama nne nyuma ya viongozi Tusker FC.

Share This Article