Anayeshukiwa kumuua mkewe apatikana amefariki kisimani

Marion Bosire
0 Min Read

Mwanaume anayeshukiwa kumuua mkewe katika kijiji cha Isongo – Butula kaunti ya Busia, amepatikana akiwa amefariki ndani ya kisima cha kanisa ya parokia ndogo ya eneo hilo.

Inadaiwa kuwa Moses mwenye umri wa miaka 61 alijirusha kwenye kisima hicho baada ya kumuua Juliana wa miaka 52 kwa sababu sizizo julikana.

Leo jumatano, polisi wameuondoa mwili huo huku wakianzisha uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha mkasa huo.

Share This Article