M23 na serikali ya Congo zakubaliana kushirikiana kurejesha amani

Makundi hayo mawili yaliafikiana jana baada ya mkutano wa mardhiano ulioandaliwa mjini Doha,Qatar.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kundi la waasi wa M23, zimekuabaliana kushirikiana kurejesha amani mashariki mwa DRC, ambayo imekabiliwa na vita kwa muda mrefu na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Makundi hayo mawili yaliafikiana jana baada ya mkutano wa mardhiano ulioandaliwa mjini Doha,Qatar.

Pande zote pia ziklikubaliana kusitisha mapigano mara moja na uchochezi.

Qatar ilianzisha mchakato wa kuleta amani nchini DRC, baada ya kuwakutanisha Marais Paul Kagame wa Rwanda, na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi, kama njia ya kumaliza mzozo huo wa muda mrefu.

TAGGED:
Share This Article