Waziri wa Fedha wa Somalia Egeh akutana na Naibu Waziri wa Marekani Meyer

Jared Ombui
1 Min Read
Bihi Iman Egeh (Kulia) na Eric Meyer (Kushoto).

Waziri wa Fedha wa Somalia, Bihi Iman Egeh, amefanya mkutano na Naibu Waziri wa Marekani wa Masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati, Eric Meyer, pembeni mwa Mikutano ya Shirika la Fedha la Ulimwenguni (IMF) na Benki ya Dunia mjini huko Washington DC

Mkutano huo uliwapa fursa ya kufanya tathmini ya programu ya mageuzi ya kiuchumi inayoendelea nchini Somalia, ambayo inaungwa mkono na IMF.

Egeh na Meyer pia walijadili njia za kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Somalia na Marekani, hasa swala la usalama na kukomesha ufadhili wa ugaidi.

Share This Article