Morocco watwaa taji ya AFCON kwa mabarubaru chini ya miaka 17

Ziyad Baha, Zakari El Khalfioui, Amine Ouahabi na Ilies Belmokhtar waliunganisha mikwaju yao minne kwa wenyeji.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Morocco walinyakua Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa mara ya kwanza jana jioni, kufuatia ushindi wa mabao 4-2 kupitia matuta ya penati dhidi ya Mali, katika fainali.

Timu zote mbili ziliambulia sarea kappa katika uwanja wa Stade El Bachir (Mohammedia), baada ya dakika 90 na kulazimu penati kupigwa kutenganisha mafahali hao wawili.

Kipa wa Morocco Zakaria Alaoui,alikuwa nyota katika hatua ya penati akipangua mikwaju miwili, huku Young Atlas, wakiibuka mabingwa baada ya kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Senegal miaka mwili iliyopita.

Ziyad Baha, Zakari El Khalfioui, Amine Ouahabi na Ilies Belmokhtar waliunganisha mikwaju yao minne kwa wenyeji.

Ivory Coast waliridhia nafasi ya tatu baada ya kuwanyuka Burkina Faso, mabao 4-1 kupitia penati kufuatia sare ya 1-1 katika mechi ya kuwania nishani ya shaba.

Share This Article