Maafisa wa polisi wamkamata Mlanguzi wa mihadarati Moyale

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akamatwa Moyale.

Maafisa wa asasi mbali mbali za usalama, wamemkamata mwanamke anayeshukiwa kuwa mlanguzi wa mihadarati  kutoka Moyale hadi Nairobi.

Jane Njeri Muigai mwenye umri wa miaka 28, alitiwa nguvni akiwa na kilo 294 za dawa za kulevya aina ya Cocaine alizokuwa ameficha katika sehemu zake za siri.

Kulingana na maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI, Njeri alikamatwa baada ya maafisa wa polisi kulisimamisha basi lililokuwa likisafiri kutoka Moyale hadi Jijini Nairobi.

Baada ya maafisa wa polisi kumpekua mshukiwa huyo aliyeonekana kuwa na wasiwasi mwingi, walipata mihadarati hiyo.

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Moyale, huku maafisa wa kukabiliana na ulanguzi na utumizi wa mihadarati wakijiandaa kumfikisha mahakamani.

TAGGED:
Share This Article