Sakata ya Mediheal: Rais Ruto amsimamisha kazi mwenyekiti wa BioVax

Tom Mathinji
1 Min Read
Upachikaji wa Fogo wapigwa marufuku katika hospitali za Mediheal.

Rais William Ruto leo Ijumaa, amemsimamisha kazi mara moja mwenyekiti wa Taasisi ya Utengenezaji na Upakiaji wa dawa Biovax, Dkt. Swarup Mishra.

Kupitia kwa taarifa, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, alisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia madai ya ukiukaji wa maadili unaohusishwa na taratibu za upachikaji wa figo katika hospitali za Mediheal, zilizoanzishwa na Dkt. Mishra.

“Agizo la kumsimamisha kazi litatekelezwa hadi uchunguzi kuhusu madai ya utovu wa maadili unaohusisha upachikaji wa figo katika hospitali ya Mediheal Eldoret, utakapotolewa,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa,” Rais alikariri kujitolea kwa serikali kukabiliana na ufisadi na kuzingatia maadili katika sekta ya afya, usalama wa umma na haki kwa waathiriwa,”.

Siku ya Alhamisi Waziri wa Afya Aden Duale, alipiga marufuku shughuli zote za upachikaji figo katika hospitali za Mediheal, kufuatia madai ya ukiukaji maadili, na akabuni kamati ya wataalam kuanzisha uchunguzi kuhusu madai hayo.

Share This Article