Mabingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi, na Beatrice Chebet, walitawazwa wanaspoti bora wa mwaka uliopita katika makala ya 21 ya tuzo za SOYA jana usiku katika ukumbi wa KICC, kaunti ya Nairobi.
Wanyonyi alinyakua dhahabu ya mita 800 katika michezo ya Olimpiki ya mwaka jana jijini Paris, Ufaransa, ikiwa na taji ya tano mtawalia kwa Kenya katika shindano hilo tangu mwaka 2008.
Upande wake Chebet alikuwa na msimu wa kufana mwaka jana akitwaa dhahabu mbili za Olimpiki katika mita 5,000 na 10,000 na pia kuweka rekodi mpya ya dunia za Dunia katika mbio za kilomita 5 na pia mita 10,000.
Mshindi wa nishani ya fedha a ya Olimpiki katika kuruka mapana, Samson Ojuka, alinyakua tuzo ya mwanamichezo bora kwa walemavu wanaume, naye Michelle Chepngetich wa urushaji kijisahani akinyakua tuzo hiyo kwa wanawake.
Kocha wa timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17, Midred Cheche, alitawazwa kocha bora wa mwaka .

Kilabu ya Nairobi City Thunder ya kikapu ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka,huku timu ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 iliyofuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka jana ikinyakua tuzo ya timu bora ya wanawake.
Mabingwa wa kitaifa wa Voliboli ya wasichana mwaka jana, Kesogon, na mabingwa wa raga ya wachezaji 15 upande kwa wavulana, Embu Boys, wakishinda tuzo za shule bora .