Courtney Henggeler aondokea uigizaji

Alifafanua kwamba hana ubaya wowote na kazi ya uigizaji lakini alitatizika na aliyokuwa akipitia kabla ya kupata kazi za uigizaji.

Marion Bosire
2 Min Read
Courtney Henggeler

Courtney Henggeler mwigizaji wa Marekani wa umri wa miaka 46 ametangaza kwamba ameondoka rasmi kwenye tasnia ya uigizaji baada ya zaidi ya miongo miwili.

Henggeler ambaye alianza kuigiza mwaka 2003 alielezea kwamba kwa miaka mingi amekuwa akipuuza sauti ambayo amekuwa akisikia kichwani mwake ikimtaka aachane na uigizaji.

Alifafanua kwamba hana ubaya wowote na kazi ya uigizaji lakini alitatizika na aliyokuwa akipitia kabla ya kupata kazi za uigizaji.

Hata baada ya miongo miwili ya uigizaji, Courtney Henggeler hakupata umaarufu sana lakini amejipatia ufuasi mpya kutokana na jukumu lake la uigizaji kama Amanda LaRusso katika kipindi cha vichekesho cha Cobra Kai kwenye Netflix.

Cobra Kai kilifikia mwisho Februari mwaka huu wa 2025 baada ya kuonyeshwa kwa muda wa miaka saba, ambapo kilikuwa na jumla ya misimu sita.

Mwisho wa mwezi Machi mwaka huu Courtney aliandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kuhusu uamuzi huo wake lakini sasa ndio umepata kuangaziwa na vyombo vya habari.

Katika chapisho hilo alielezea kwamba aliwasiliana na maejenti wake wanaohusika na kumtafutia kazi za uigizaji akawajuza kwamba ameamua kustaafu.

Alizungumzia uhusika wake kwenye Cobra Kai akisema, “Nilikuwa kwenye kipindi hicho. Kipindi kilichofanikiwa sana. Nilitengeneza pesa. Sura yangu iliwekwa kwenye mabango makubwa barabarani nilivyotamani kwa zaidi ya miaka 20.”

Mwigizaji huyo aliendelea kusema kwamba amechoka kutafuta na kufuata hila ambayo haijiishara kwamba alitarajia kuafikia ufanisi mkubwa hata zaidi katika uigizaji lakini mambo yakawa tofauti.

Alielezea kwamba kitu ambacho awali alikitizamia kuwa cha lazima, ambacho alifanya kwa hiari na hata kukisherehekea kiligeuka na kuwa mzigo na kwamba hataki tu kuwa sehemu ya mashine.

Alipoulizwa anachotaka kufanya baada ya kuondokea uigizaji, Coutney alisema kwamba angependa kuwa mashine yenyewe ishara kwamba huenda akaingilia maandalizi ya filamu.

Share This Article