Mpelelezi asimamishwa kazi baada ya kuonekana uchi kwenye video

Alikodishwa kuigiza kwenye video ya muziki, waandalizi wakidai hawakujua yeye ni afisa wa polisi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mpelelezi wa kike anayefanya kazi katika idara ya polisi ya New York nchini Marekani almaarufu NYPD, amesimamishwa kazi baada ya kuonekana kwenye video ya muziki akicheza uchi.

Melissa Mercado ambaye alijipatia umaarufu mitandaoni kufuatia kuchapishwa kwa video hiyo, ameondolewa kwenye upelelezi wa kesi za uhalifu wa kingono alizokuwa akishughulikia.

Hatua hiyo inatoa fursa kwa maafisa wa polisi kufanya uchunguzi kuhusu tabia yake.

Afisa huyo ambaye anaaminika kuwa mpelelezi stadi amesimamishwa kutoka kutekeleza majukumu yake ya kawaida ya kuchunguza kesi za uhalifu wa kingono.

Kinachochunguzwa kwa sasa ni kuona iwapo aliwasilisha stakabadhi za kuonyesha hakuwa kazini wakati wa kuandaliwa kwa video hiyo. Kila afisa katika NYPD huhitajila kuwasilisha stakabadhi kama hizo iwapo wanashughulikia kazi nyingine.

Kwa sasa haijulikani iwapo Melissa alikiuka sheria za NYPD kwakuonekana kwenye video ya wimbo uitwao ‘Doin That’ wa mwanamuziki S-Quire ambapo alikuwa amevaa sidiria na kisuruali kidogo.

S-Quire na mwelekezi wa video hiyo walisema kwamba walielekezwa kwa Mercado na shirika moja linalohusika na usajili wa waigizaji na hawakufahamu kwamba yeye ni afisa wa polisi.

Share This Article