Rais Ruto ahudhuria mazishi ya Chebukati Trans Nzoia

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kuzikwa nyumbani kwake Trans Nzoia.

Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi na wananchi ambao wanahudhuria mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, katika kaunti ya Trans Nzoia.

Chebukati alifariki Februari 20, katika kile familia yake ilisema alikumbwa na mshtuko wa moyo alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Jijini Nairobi.

Aidha msemaji wa familia Eric Nyongesa, alisema Chebukati aligonjeka saratani ya akili, ambapo alifanyiwa upasuaji mara mbili.

Wafula Chebukati, alisimamia chaguzi tatu hapa nchini ambazo ni; Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017, marudio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Upeo, na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.

Alistaafu wadhifa wa mwenyekiti wa IEBC, baada ya kukamilisha muhula wake wa miaka 6 Januari 17, 2023. Alifariki akiwa na umri wa miaka 63.

Viongozi wengine wanaohudhuria mazishi hayo ni pamoja na waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, Spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula, Spika wa Senate Amason Kingi, Gavana wa Bungoma Ken Lusaka, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na katibu wa usalama wa taifa Raymond Omollo miongoni mwa wengine.

Share This Article