NACADA wanasa Shisha, Lang’ata

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Shirika la kukabiliana na matumizi ya mihadarati (NACADA), walinasa makasha 16 ya katoni nyingine 106 za kileo cha Shisha kwenye msako uliofanyika katika kilabu cha Paris Lounge mtaani Lang’ata.

Watu wawili pia walikamatwa wakati wa msako huo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Akizungumza wakati wa msako huo Afisa wa utekelezaji wa sheria katika shirika la NACADA James Koskey, alitoa onyo kali kwa wanaokiuka sheria kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Matumizi ya sigara ya mvuke maarufu kama Shisha yalipigwa marufuku nchini mwaka 2017.

Share This Article